top of page

SHULE YA BIBLIA 

Utangulizi

Kitengo cha Shule ya Biblia kwa njia ya posta kwa jina lingine Sauti ya Unabii (Voice of Prophecy), ni idara muhimu sana katika taasisi ya habari ya Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (Tanzania Adventist Media center). Asasi nyingine za habari za kanisa yaani Adventist World Radio, Morning Star Radio na Morning Star Television, zote zimejengwa na zinaendelea kujengwa juu ya misingi asili ya Shule hii ya Biblia ambapo masomo ni yale yale, ujumbe ni ule ule ila ukitolewa kwa mbinu na namna tofauti tofauti

 

 

Masomo Yanayotolewa

 

Kwa sasa shule ya Biblia kwa njia ya Posta inatoa masomo ya aina mbili kwa wanafunzi mbali mbali ndani na nje ya kanisa:

 

I ) masomo ya kawaida ya kuanzia

ii) masomo ya kawaida hatua ya pili.

 

Masomo ya hatua ya kwanza (regular) huhitimishwa kwa kawaida baada ya kujifunza masomo 20, wakati yale ya hatua ya pili (advanced) huhitimishwa baada ya mwanafunzi kujifunza masomo 21.

 

 

Matumizi ndani ya  Makanisa

 

Masomo yamekuwa yakitumika makanisani katika namna nyingi. Kwanza masomo yanatumika kuwasomesha na kukomaza washiriki wapya na wanafamilia. Kando ya hiyo, masomo Sauti ya Unabii yamekuwa yakitumika kuwasomesha wale walio nje ya Kanisa hasa marafiki, ndugu na majirani za washiriki au kanisa kupitia idara za Shule ya Sabato na Sauti ya Unabii. Vile vile masomo ya Sauti ya Unabii yanatumika na idara ya huduma za washiriki kama sehemu ya utaratibu wa kuandaa mahubiri ya hadhara (effort). Masomo yanatumiwa kujenga urafiki na pengine kuwaandaa watu watakaovunwa katika mikutano hiyo, au hata mapema kabla ufanyikaji wake. Watu binafsi pia wanafadhili usomeshwaji wa watu moja moja au vikundi mbali mbali vilivyolengwa kufikiwa kwa njia hiyo.

 

Upatikanaji wake, Bei na Uwakala

 

Masomo ya Sauti ya Unabii kwa sasa yanapatikana katika ofisi kuu ya TAMC iliyoko Mikocheni jijini Dar es Salaam.

 

Mtu binafsi, kanisa mahalia au ofisi ya Field/Konferensi yaweza kufanya mawasiliano kupitia namba zifuatazo ili kupokea masomo;

 

Simu ya kiganjani: 0754983861.

Email:...........@tamc.or.tz

 

 

 

 

Nukuu za kibiblia

 

Isaya  8:19, 20:19

"Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong'ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai? 20 Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi".

 

Ufunuo  12:17

"Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.Uf 19:10 Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii".

 

2Petro 1:19-21:19

"Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing'aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu. 20 Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. 21 Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu".

 

2Timotheo 3:14-17:14

"Bali wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao; 15 na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu. 16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;17 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema".

 
mtizamo wetu

kutangaza injili hata miisho ya dunia "Enendeni ulimwenguni kote mkawafanye wote kuwa wanafunzi wangu Mat 28:19 "

  • Wix Facebook page
  • Twitter Classic
  • morning radio.jpg

2014© for Tanzania Adventist Media Center

Tunapatika mikocheni B
bottom of page