VITUO CHINI YA VOP/TAMC
Sauti ya unabii
Mategemeo ya VOP ni kutangaza injili," Nendeni na muwafanye mataifa yote kuwa wanafunzi kwa kuwabatiza kwa jina la baba na la mwana na la Roho Mtakatifu, huku mkiwafundisha yote niliyowaelekezeni; Nami ni pamoja nanyi hata mwisho wa dahari Mat 28:19,20". Hapa Tanzania huduma za VOP zilianza 1969. " Inafanya kazi kama shule ya Biblia .
Radio ya kisabato duniani
Radio ya kisabato duniani Morogoro ilianzishwa na kuanza matangazo yake ya kiswahili mwaka 1997. Matangazo kwa lugha ya kimasai yalianza kurushwa 2001. Matangazo yetu yanarushwa kila siku kutokea Africa ya kusini kwa mawimbi mafupi kwenye mita bendi 2,25 au 31 kuanzia saa 8:00-8:30 kwa lugha ya kiswahili na 8:30-9:00 kwa lugha ya kimasai. Wasiklizaji wetu wa Afrika Mashariki wamekuwa wakitutumia ujumbe mfupi kuonesha ukubali wao wa ubora wa vipindi vyetu.
Morning star Redio
kituo cha redio cha Morning star kilianza matangazo yake mwaka 2013.Kituo kinarusha matangazo yake tokea Mikocheni ,jijini Dar es salaam pia inasikia katika mikoa ya Tanga,Mwanza, Mara,Kigoma, Mbeya,Iringa,Morogoro,Arusha na Tabora. Vile vile kinasikia katika sehemu chache za mikoa ya Pwani, Kilimanjaro,Rukwa,Kagera na Zanzibari. Kituo kinatangaza ulimwengu mzima kupitia satelite na intaneti. Kituo kinasikika kila siku angalau kilomita za mraba 3,000,000 nchini Tanzania.
Morning star Televisheni
Mwaka 2007 mkutano mkuu wa Union ya Tanzania iliteua VOP/TAMC kuanzisha taratibu za namna ya kuanzisha kituo cha utangazaji kupitia televisheni. Kituo hakikuanza shughuli zake hadi ilipofika mwaka 2013 ambapo Kituo kilianza utengenezaji wa vipindi . Serikali ya jamhuri ya Muungano ya Tanzania ilitoa leseni isiyo ya kibiashara kwa ajili ya kituo tarehe 26.02.2014. Kwa sasa TAMC inachukua kila hatua kuhakikisha kituo kinaanza kurusha matangazo yake mapema mwezi wa tano.
